Karibu kwenye UBCtv-Homepage !

Ukurasa huu ndio msingi wa UBC katika mtandao. Unatoa wasaa wa kutuelewa sisi na pia kushiriki katika baadhi ya miradi. Ili kuelewa vizuri pointi zote kutoka mwanzoni, tunapata majibu kwa FAQ hii ifuatayo:

Hivi huu ukurasa unatoa nini? - UBC ni nini? - Ense-Fighter ni nini?

Übersetzt von: Romwald Haule

Huu ukurasa unatoa nini?

Kwanza kabisa unatoa utofauti: Tunajitambulisha wenyewe na filamu zetu fupifupi. Huko nyuma kuna taarifa kuhusu video zetu, taarifa kuhusu mipango ya sasa na maonyesho ya picha yanayotokana na filamu zetu. Nusu ukurasa wa pekee umetolewa kwa ajili ya kutoa historia ya Ense-Fighter, pamoja na picha, mchezo wa karata na filamu. Cha muhimu pia ni jinsi ukurasa wetu unavyofanya kazi, ambao kwao kila mmoja anaweza, kwa mfano kushiriki katika historia ya miradi yetu au kwa kufungua na kuona makusanyo yetu. Zaidi ya hayo, kuna uwezekano wa kuipata picha kutoka kwenye desktop, na pia kuwaagiza wafanyabiashara wa UBC. Kumbuka: unakaribishwa sana kushiriki!

UBC ni nini?

UBC ni ufupisho wa United BrainCompany. Katika jina hilo sisi, kikundi wazi, tunatngeneza matoleo ya video na filamu fupifupi toka mwaka 1991. Tukiwa na asili kutoka kwa waanzilishi wa UBC - Marco Euskirchen, Karl-Heinz Laschke na Michael Osterhaus, ambao kwa kipindi hicho walikuwa katika shule moja - tukapanua UBC mpaka kufikia watu sita wa uhakika, na marafiki mbalimbali na wahisani. Hata hivyo mtu mmoja tu ameweza kuifanya hobby yake kuwa kazi na sasa anafanya kwenye studio ya Tv. Hobby yetu ya pamoja ya kutengeneza filamu imeendelezwa nasi kwa muda sasa wa miaka kumi.

Ense-Fighter ni nini?

Mmoja wa wacheza filamu tulio nao ni ENSE-FIGHTER; ambaye ni wa kubuni tu, ni mmoja mashuhuru wa manispaa ndogo ya Ense huko Ujerumani. Katika vijiji hivi tunavyotoka, yeye ni mpiganiaji asiyechoka kwa ajili ya mambo mazuri na ubora wa manispaa na anaona kuwa adui wake mkubwa, shetani Dr. DUUM hatafaulu kuiteka Ense. Mwaka 1996/7 tulitengeneza filamu moja nzuri kwa jina la Ense-Fighter, ilikuwa ni dokumenti ya toleo ndefu la filamu ambalo halijawahi kutokea. Kadiri ya historia ya Ense-Fighter, kuna wafuasi kama 20, wote ambao tutawatambulisha katika dokumenti ya kubuni ya Ense-Fighter ambayo ipo katika matengenezo. Sehemu za wafuasi hao wote zipo tayari katika homepage ili wote waweze kusoma.